Type Here to Get Search Results !

SHIRIKA LA MAPAO LAENDELEA KUWAFIKIA WANAFUNZI KWA KUWAPA ELIMU

Wanafunzi Shule ya Msingi Luvulunge iliyopo kata ya Isapulano Wilayani Makete Mkoani Njombe wameanza kunufaika na Elimu ya wasaidizi wa Kisheria inayotolewa na Shirika la Makete Paralegal Organisation(MAPAO)
Mandhari ya Shule ya Msingi Luvulunge iliyopo kijijini hapo kata ya Isapulano Wilayani Makete yenye wanafunzi 134 kuanzia Darasa la kwanza mpaka Darasa la sita

Mkurugenzi wa Shirika hilo la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete DENIS SINENE amesema utoaji wa Elimu hiyo kwa Wanafunzi ni katika kuwasaidia watoto kuwa na Misingi bora ya Elimu na kujua haki zao za Msingi ikiwa ni pamoja na wao kutambua wajibu wao

Mkurugenzi wa Shirika hilo la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete DENIS SINENE Ametoa Maelezo hayo wakati wa kuanzisha Klabu ya Wasaidizi wa Kisheria Shuleni hapo ikiwa ni Mwendelezo wa kuanzisha Klabu hizo kwenye Shule za Sekondari na Msingi Wilayani hapa

Akizungumza na wanafunzi hao Denisi Sinene amesema “Tunafanya kazi za kuisaidia jamii ya wanaMakete ikiwa ni pamoja na wazazi wenu,ndugu zetu ikiwa ni pamoja na ninyi watoto mnapokuwa na Matatizo kwenye masuala madogomadogo ya kisheria”

“Jukumu letu tunaelekeza,tunashauri,tunapatanisha,tunaonya,tunatetea haki za walemavu,tunafundisha sheria na haki za watoto,wazee na wanawake kwenye kata zote ndio kazi tunazozifanya”Aliongeza Sinene

Mkurugenzi huyo ameelezea dhamira na Lengo la kuwepo kwa Wasaidizi wa Kisheria Wilayani hapa pamoja na kuwataka watoto kuwa watiifu kwa wazazi wao na Jamii inayowazunguka
Denis Sinene amesema “Dhamira ya MAPAO ni kuwa na Jamii inayotambua haki za Binadamu na ninyi ni miongoni mwa Jamii,sasa tunataka jamii hii ijue haki,kwa hiyo sasa Makusudi ya MAPAO inataka Jamii ijue haki na ninyi pia mjue haki mbalimbali za Binadamu nanyi muwe na uelewa kuhusu haki zenu”

Kwa Upande wake Mjumbe wa Bodi ya MAPAO Ndg.Nahumu Tweve amesema wanafunzi hao wakiendelea kupatiwa Elimu hiyo mara kwa mara Taifa litakuja kuwa na Vijana waadilifu na kuyaishi mema wakati wote

Nahumu Tweve  amesema “Wapo wahalifu ndio maana ipo Sheria sasa ninyi mkilelewa katika Misingi yenye Maadili naamini mtakuwa wazalendo,waadilifu,wenye unyoofu na baadaye tutakuwa na Taifa lenye watu waelewa sasa ninyi shule ya Msingi Luvulunge tunategemea mtakuwa mfano mzuri kwa watoto kutoka shule zingine ndani na nje ya Wilaya ya Makete kwa kuwa na watoto waadilifu,wanaojua sheria na wajibu wao”

“Tunategemea hamtasumbua walimu,hamtasumbua wazazi,hamtalisumbua Taifa kwa sababu mtakuwa mmeshaelewa wajibu wenu katika Jamii na hapa shuleni mtayaishi yale tutakayokuwa tunawafundisha,na nyie mkawe mnawafundisha wengine huko nyumbani”

Mkurugenzi wa Shirika hilo la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete DENIS SINENE amesema watoto wanatakiwa kujitambua kwa kujua wajibu wao kwa wazazi huku Klabu ya wasaidizi wa Kisheria iliyoundwa hii leo shuleni hapo ikiwa na wajumbe(Wanafunzi) Zaidi ya 40

Shirika la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete MAPAO limeanzisha Klabu 2 za Wasaidizi wa Kisheria kwa Wanafunzi,Klabu moja kutoka shule ya Sekondari Iwawa kata ya Iwawa na Klabu nyingine imeanzishwa leo shule ya Msingi Luvulunge iliyopo kata ya Isapulano na hii ni katika Mpango endelevu wa kutoa Elimu ya Kisheria kwa wanafunzi shule zote za Msingi na Sekondari Wilayani hapa

Picha mbalimbali kuhusu kilichofanyika leo Shuleni hapo Tazama hapa chini

 Wanafunzi wa shule ya Msingi Luvulunge wakisiliza kwa Umakini Elimu iliyokuwa ikitolewa na Viongozi wa MAPAO


 Kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Luvulunge Frolida Ilomo akitambulisha wageni kutoka Shirika la MAPAO waliotembelea shuleni hapo na kutoa Elimu ya wasaidizi wa Kisheria

 Mkurugenzi wa Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete Denis Sinene akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Luvulunge

 Mkurugenzi wa Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete Denis Sinene akiimba wimbo wa MAPAO pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Luvulunge
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa MAPAO Denis Sinene,katikati ni Mjumbe wa Bodi ya Mapao akizungumza na wanafunzi shuleni hapo


 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi MAPAO Frolida Ilomo akizungumza jambo
Huu ni ubao wa Mahudhurio ya wanafunzi shule ya Msingi Luvulunge kwa wiki hii

Post a Comment

0 Comments

Top Post Ad

Below Post Ad