Type Here to Get Search Results !

FAHAMU MAJUKU YA MWENYEKITI WA KIJIJI NA MIPAKA YAKE!

Katibu katika tovuti ya Shirika la kudhihirisha Uzalendo MAPAO leo tutawaletea elimu ya majuku ya baadhi ya viongozi ngazi ya kijiji kwa Majukumu na kazi za Mwenyekiti wa kijiji,Mwenyekiti wa Kitongoji na Mwenyekiti wa Mtaa.

 

MAJUKUMU NA KAZI ZA MWENYEKITI WA KIJIJI

(i) Atakuwa ndiye Mkuu wa Serikali ya Kijiji;

(ii) Atakuwa na wajibu wa kuitisha na kuongoza mikutano yote ya Halmashauri ya kijiji, pamoja na Mikutano Mikuu ya Kijiji. Lakini endapo Mwenyekiti hayupo katika mkutano wowote, wajumbe wa mkutano unaohusika wanaweza kuchagua Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo;

(iii)Atakuwa mwakilishi wa kijiji kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata;

(iv) Atawahudumia kwa usawa wanakijiji wote, bila kujali tofauti za Kisiasa, Kijinsia au za Kidini;

(v) Atakuwa mfano wa uongozi bora na utendaji bora wa kazi, kwa kuwa na shughuli zake mwenyewe za kujitegemea, ambazo zaweza kuigwa na wanakijiji wenzake.


MAJUKUMU NA KAZI ZA MWENYEKITI WA MTAA

(i) Kuwa Mwenyekiti wa Mikutano yote ya Kamati ya Mtaa na Mkutano wa Mtaa;

(ii) Kusuluhisha migogoro midogomidogo ambayo haistahili kuitisha mkutano wa Kamati ya Mtaa au kupelekwa kwenye Baraza la Kata au Mahakama;

(iii)Kuwa msemaji wa Mtaa;

(iv) Kuwaongoza na kuwahimiza Wakazi wa Mtaa washiriki shughuli za maendeleo, sherehe za Taifa, Mikutano ya hadhara itakayoandaliwa na Mtaa, Halmashauri ya Mji Manispaa au Jiji na Serikali;

(v) Kuwakilisha Mtaa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata;

(vi) Kutekeleza kazi atakazopewa na Kamati ya Mtaa na Mkutano wa Mtaa na Kamati ya Maendeleo ya Kata;

(vii) Kusimamia utekelezaji wa kazi na Majukumu ya Kamati ya Mtaa;

(viii) Kusimamia utunzaji wa rejesta ya wakazi wote wa Mtaa.


Shirika la kudhihirisha Uzalendo hutoa elimu ya msaada wa kisheria bure,hatuwezi kukuwakilisha mahakamani lakini tunao washirika ambao tunaweza kukuunganisha nao karibu kwa Maswali katika mitandao yetu tukujibu haraka


. MAJUKUMU NA KAZI ZA MWENYEKITI WA KITONGOJI

(i) Kutunza rejista ya wakazi wa kitongoji na nyaraka nyingine muhimu zinazohusu maendeleo ya kitongoji kwa jumla ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za vizazi na vifo;

(ii) Kusimamia shughuli za ulinzi na usalama wa watu na mali zao waishio katika eneo lote la kitongoji;

(iii)Kuhamasisha ulipaji wa kodi na ushuru mbalimbali, kama utakavyoamuliwa na kuwekwa mara kwa mara na Halmashauri ya Kijiji, Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji;

(iv) Kusimamia katika eneo lake suala zima la Hifadhi ya mazingira hususan vyanzo vya maji n.k.;

(v) Kusimamia suala la afya katika eneo lake ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kampeni za afya za Kitaifa, Kimkoa au Kiwilaya dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, na hasa, Vita dhidi ya UKIMWI;

(vi) Kusimamia utekelezaji wa kanuni za kilimo na ufugaji bora ili kuinua hali ya lishe na uchumi wa wakazi wa kitongoji;

(vii) Kufuatilia na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapatiwa nafasi na kushirikiana na viongozi wa shule katika udhbiti utoro shuleni;

(viii) Kuhamasisha elimu ya watu wazima;

(ix) Kusimamia na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji katika kutekeleza shughuli za kujitegemea;

(x) Kusuluhisha migogoro midogo midogo isiyostahili kushughulikiwa na Mabaraza ya Kata au Mahakama;

(xi) Kuwakilisha kitongoji katika Serikali ya Kijiji;

(xii) Kuwaongoza na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji washiriki katika sherehe za Taifa na mikutano ya hadhara itakayoandaliwa na kuitwa na Serikali au Halmashauri;

(xiii) Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na Halmashauri ya Kijiji, Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji.


Post a Comment

0 Comments

Top Post Ad

Below Post Ad