Type Here to Get Search Results !

JE! UNAJUA MIPAKA YA KIKAZI YA WATENDAJI WA KIJIJI NA KATA? SOMA HII LEO

Ahsante kwa kutembelea tovuti yetu kwa ajili ya kupata maarifa na elimu ya sheria leo tutazungumzia Majukumu na mipaka ya maafisa watendaji wa vijiji na kata JE! una swali lolote usisite kutuuliza Shirika la Kudhihirisha Uzalendo MAPAO 

MAJUKUMU YA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI

(i) Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.

(ii) Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya kijiji

(iii)Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.

(iv) Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya kijiji

(v) Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.

(vi) Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Kijiji.

(vii) Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata.

(viii) Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.

(ix) Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.

(x) Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.

(xi) Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.

(xii) Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika kijiji.


MAJUKUMU YA AFISA MTENDAJI WA KATA

(i) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata

(ii) Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini.

(iii)Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.

(iv) Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na vitongoji.

(v) Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Kata.

(vi) Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake.

(vii) Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya Kata.

(viii) Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.

(ix) Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.

(x) Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.

Je! una swali lolote kuhusu Sheria mbalimbali,umekuwa ukijitatizo katika masuala ya Ndoa,mirathi na mengineyo usisite kuwasiliana nasi kupitia mitandao yetu ya kijamii kwa kubofya hapa chini.


Post a Comment

0 Comments

Top Post Ad

Below Post Ad