Type Here to Get Search Results !

JE! WAJUA KWANINI NI MUHIMU KUWA NA MKUU WA MKOA? FAHAMU MAJUKUMU YAKE HAPA

Tunaendeleo kutoa elimu na kuisaidia jamii kuhusu masuala ya Kisheria ambapo unaweza kujiuliza bure bila kutozwa garama yoyote tupigie simu au wasiliana nasi katika kurasa za mawasiliano hapo chini au kisanduku cha barua pepe!

 MAJUKUMU YA MKUU WA MKOA

(i) Kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa (Katiba 1977, ib. 61(4))

(ii) Kuwa mwenyekiti wa RCC inayotoa ushauri kuhusu masuala mbalimbali mkoani mwake (RAA No 19/1997).

(iii) Mhimili wa Halmashauri za wilaya (LG Finance Act No 9/1982)

(iv) Mhimili msaidizi wa Halmashauri za Miji iliyoko katika mkoa wake (LG (Urban Authorities) Act No 8/1982)

(v) Kumwekakizuizini kwa saa 48 mfululizo mtu anayehisiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu naamani (Regional Admin Act No 19/1977)

(vi) Kuongoza Kamati ya Mkoa ya maombi ya leseni za magari (Motor Vehicles, Registrations, Acquisitions and Dispositions Act No 5/1972, ib 24(2))

(vii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa inayoshughulikia uteuzi wa vijana wanaojiunga na jeshi la kujenga taifa (National Service Act No 16/1964)

(viii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978)

(ix) Kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1)

(x) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)

(xi) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya utoaji wa leseni za magari na uchukuzi (Transport Licensing Act No 1/1973)

(xii) Kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100)

(xiii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani kwake ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani wakati wote na kuishauri serikali ipasavyo (National Defence Act No 24 1966)

(xiv) Kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18)

Unaweza kubofya Tangazo letu la Msaada wa Kisheria na kutufikia kupitia Whatsapp haraka zaidi bila kuandika number ya simu. Tafadhali kama unasoma ujumbe huu tafadhali shere ujumbe huu uwafikia wahitaji wa Msaada Kisheria.

MAJUKUMU YA KATIBU TAWALA WA MKOA

(i) Kuratibu shughuli zote za utawala kwenye sekretariati ya mkoa

(ii) Kuwa mshauri mkuu wa mkuu wa mkoa katika masuala ya sharia,kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za serikali za mitaa.

(iii) Kuwa katibu wa Kamati ya ushauri ya mkoa (RCC)

(iv) Kuwa mkuu wa watumishi waserikali kuu katika mkoa

(v) Kushauri na kuratibu upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya serikali za mitaa

(vi) Kuwajibika kwa fedha zote zitakazopelekwa mkoani kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mipango ya sekretariati ya mkoa na ofisi za wakuu wa wilaya

(vii) Kuwa afisa mhasibu wa fedha za serikali kuu mkoani

(viii) Kuwa mwenyekiti wa bodi za zabuni ya mkoa

(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Utumishi serikalini (KAMUS)

(x) Kuwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya wataalamu katika sekretariati ya mkoa na kamati nyingine zitakazotokea kwa dharura

(xi) Kupokea na kuchambua takwimu na taarifa za utekelezaji zinazotoka kwenye halmashauri na mashirika mbalimbali

(xii) Kufuatilia upatikanaji na usambazaji wa pembejeo na zana muhimu za kazi ikiwa ni pamoja na mahitaji mengine kama vile wataalamu na fedha.


Post a Comment

0 Comments

Top Post Ad

Below Post Ad