Type Here to Get Search Results !

LEO TUJIFUNZE KUHUSU MAJUKU YA MKUU WA WILAYA NA KATIBU TAWALA WILAYA NI YEPI?

Siku zote Elimu haina Mwisho,wengine wanasema Elimu ni Bahari basi leo tujikumbushe kuhusu Majukumu ya Viongozi ngazi ya wilaya yaani Mkuu wa Wilaya na katibu Tawala wa Wilaya,Je! wanapaswa kufanya nini na wanawajibika kwa nani? karibu sana katika Tovuti hii kwa Elimu zaidi ya Msaada wa Kisheria. 

MAJUKUMU YA MKUU WA WILAYA

(i) Kumweka mtu kizuizini kwa muda wa saa 48 mfululizo iwapo atashukiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu na Amani (Sheria ya tawala za mikoa Na 19/1997)

(ii) Kufungisha ndoa za serikali (Law of Marriage Act No 5/1971)

(iii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978)

(iv) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1)

(v) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)

(vi) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100)

(vii) Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18)

(viii) Kuwa mhimili msaidizi wa Halmashauri za Wilaya (Sheria Na 7/1982).

(ix) Kuwa mwenyekiti wa Kamati mbalimbali zitakazoundwa Wilayani.

(x) Kuhudhuria vikao vya Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kamamjumbe

(xi) Kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi

(xii) Kumsaidia Mkuu wa Mkoa katika kuzisimamia Halmashauri za Wilaya na kuhakikisha kuwa zinatoa huduma nzuri kwa wananchi na kwa ufanisi

(xiii) Kuziwekea Halmashauri za Wilaya mazingira mazuri na kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kulingana na sera za serikali.

(xiv) Kutekeleza majukumu yote atakayopewa kisheria au kukasimiwa na Mkuu waMkoa.

Ahsante kwa kutembelea Tovuti hii kama unausoma ujumbe huu tambua tunadhamini mchanago wako wa kusoma tulichokichaapisha,tembelea kusoma taarifa mbalimbali na tuulize suala lolote kuhusu sheriaa tutakusaidia bure Ahsante

MAJUKUMU YA KATIBU TAWALA WA WILAYA

(i) Kumshauri Mkuu wa Wilaya katika masuala yanayohusu ulinzi na usalama

(ii) Kumshauri Mkuu wa Wilaya katika masuala yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya sherehe na dhifa za kitaifa

(iii) Kumshauri Mkuu wa Wilaya katika masuala yanayohusu malalamiko ya wananchi

(iv) Kumshauri Mkuu wa Wilaya katika masuala yanayohusu uwekaji wa mazingira bora ya kuziwezesha Halmashauri za Wilaya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sera za serikali.

(v) Kuwa Kiongozi Mkuu wa Utawala katika ngazi ya Wilaya.

(vi) Kuwa Msajili wa Vizazi na Vifo.

(vii) Kuwa msajili wa ndoa.

(viii) Kuandaa makadirio ya matumizi ya Wilaya.

(ix) Ushughulikia masuala ya itifaki Wilayani

(x) Kuratibu harakati za kupambanana dharura za maafa Wilayani.

(xi) Kutekeleza majukumumengine kama atakavyoagizwa na Mkuu wa Wilaya na Katibu Tawala wa Mkoa.


Post a Comment

0 Comments

Top Post Ad

Below Post Ad