Type Here to Get Search Results !

NINI MAANA YA "𝗔𝗡𝗔 𝗞𝗘𝗦𝗜 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗕𝗨" SOMA HAPA

 Hii ni hatua tu katika kesi yoyote ya Jinai na sio uamuzi wa mwisho katika kesi. ( Hatua hii humaliza kesi endapo washtakiwa wakikutwa hawana kesi ya kujibu).


Kwa mujibu wa kifungu cha 293 (2) cha SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI SURA YA 20.

Endapo ushahidi wa upande wa mashtaka umekamilika na mahakama inaona upande wa mashtaka wametoa ushahidi unaoashiria kuwepo jinai, mahakama itatamka kuwa washtakiwa wana "kesi ya kujibu".

Baada ya hapo washtakiwa watafahamishwa haki yao ya kuanza utetezi, na mawakili au washtakiwa wenyewe watataja idadi ya mashahidi watakaokuwa nao na mahakama itapanga siku ya kuanza kusikiliza utetezi.

CC:JUNGU LA SHERIA.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Top Post Ad

Below Post Ad