Type Here to Get Search Results !

WANANCHI KINYIKA JITOKEZENI KUPIGA KURA

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Manifestation of patriotism organization (MAPAO) Shirika linalo jishughulisha na Utoaji wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kwa ufadhilii wa Lsf.Mch.Denis Sinene anawaomba Wananchi na wanachama wote wa vyama vya siasa viongozi wa Taasisi zote kujitokeza na kuhudhuria katika mikutano ya utoaji Elimu ya Mpiga kura katika uchaguzi mdogo wa Diwani kata ya Kinyika uchaguzi utakao fanyika Tarehe 13/7/2023  Alhamisi.              

Mkurugenzi wa shirika la MAPAO akitoa elimu kwa njia ya redio kituo fm

Elimu hiyo itatolewa katika Kata ya Kinyika kwa vijiji vyote na Shirika hilo la MAPAO na wadau wengine wa Tume ya Uchaguzi. Shiriki elimu hiyo ili ujue haki yako ya kupiga kura na kuchagua kiongozi bora atakaye kusaidia kuleta maendeleo katika kata Yako.

ELIMU YA MPIGA KURA

Mwaka 2020 Shirika la MAPAO kwa Kupitia Tume ya taifa ya Uchaguzi shirika lilipata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Raisi, Wabunge na Madiwani Katika Wilaya ya Makete Kazi iliyofanywa kwa ufanisi mkubwa na watu walijitokeza kwa wingi kupiga kura.

Mwaka huu wa 2023 Shirika limepata neema tena ya kupata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura katika uchaguzi Mdogo wa madiwani kata 14 na mapao imepewa kutoa elimu katika kata ya Kinyika - Makete.

Nini maana ya Elimu ya mpiga kura:Ni Elimu inayotolewa kwa wananchi wote ikiwa na lengo la kuwasadia wananchi kupata uelewa kuhusiana na sheria, Taratibu na Kanuni katika uchaguzi.

"Elimu hii ni elimu isio na mlengo au hisia za ubaguzi wa  kidini,kisiasa na ukabila.Elimu ya mpiga kura ni maelekezo ya huyu mpiga kura Wapi atatakiwa kwenda kupiga kura,Muda,na lini atapiga kura na umuhimu wa kushiriki kupiga kura" amesema Sinene

'Kupiga kura ni haki kwa kila mtu aliye kidhi vigezo sifa hivyo elimu ya mpiga kura ni kumkumbusha mpiga kura kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba kwa kujitokeza na kushiriki Kuchagua Viongozi wao watakao waongoza kwa lengo la kujenga Demokrasia na utawala bora katika kata wilaya na nchi nzima' amesema

Hivyo ni muhimu sana kujitokeza kupiga kura usubiri kuamuriwa na wengine kura yako ni ya muhimu sana

Post a Comment

0 Comments

Top Post Ad

Below Post Ad